Matthew 22:1-6

Mfano Wa Karamu Ya Arusi

(Luka 14:15-24)

1 aIsa akasema nao tena kwa mifano, akawaambia, 2 b“Ufalme wa Mbinguni unaweza kufananishwa na mfalme mmoja aliyemwandalia mwanawe karamu ya arusi. 3 cAkawatuma watumishi wake kuwaita wale waliokuwa wamealikwa karamuni, lakini wakakataa kuja.

4 d“Kisha akawatuma watumishi wengine akisema, ‘Waambieni wale walioalikwa kwamba nimeandaa chakula. Nimekwisha kuchinja mafahali wangu na vinono, karamu iko tayari. Karibuni kwa karamu ya arusi.’

5“Lakini hawakuzingatia, wakaenda zao: huyu shambani mwake na mwingine kwenye biashara zake. 6Wengine wao wakawakamata wale watumishi wake, wakawatesa na kuwaua.
Copyright information for SwhKC